Acts 10:25-28

25Petro alipokuwa akiingia ndani, Kornelio alikuja kumlaki, akaanguka miguuni pake kwa heshima. 26 aLakini Petro akamwinua akamwambia, “Simama, mimi ni mwanadamu tu.”

27Petro alipokuwa akizungumza naye akaingia ndani na kukuta watu wengi wamekusanyika. 28 bAkawaambia, “Mnajua kabisa kwamba ni kinyume cha sheria yetu Myahudi kuchangamana na mtu wa Mataifa au kumtembelea. Lakini Mungu amenionyesha kwamba nisimwite mtu yeyote kuwa najisi au asiye safi.
Copyright information for SwhKC